Home Uncategorized Yanga Yaogopa Kuvunja Mikataba na Wachezaji Wake Kuhofia Hasara.

Yanga Yaogopa Kuvunja Mikataba na Wachezaji Wake Kuhofia Hasara.

1
0

Yanga Yaogopa Kuvunja Mikataba na Wachezaji Wake Kuhofia Hasara

Baada ya wachezaji baadhi wa Yanga kutoonekana dimbani kwa muda mrefu, uongozi wa Yanga umesema unahofia kuvunja nao mikataba kwa hofu ya kupata hasara.


Donald Ngoma na Amis Tambwe ni miongoni mwa wachezaji walioshindwa kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kuwa wana hofu ya kuvunja nao mikataba kwasababu itawalazimu kuwalipa fedha za uvunjaji.

Kauli ya Mkwasa imekuja kutokana na klabu hiyo kutokuwa vizuri kiuchumi kwa sasa tangu Mwenyekiti wao Yusuph Manji kutangaza kujiuzulu nafasi yake.

Kutokuwepo kwa wachezaji hao kumechangia kikosi hicho kushindwa kupata matokeo yasiyo mazuri kwenye ligi msimu huu kwani huduma yao ina muhimu mkubwa ndani ya timu.

Previous articleDiamond Aingia Location na Miri Ben-Ari UK Kutengeneza Video ya Baila
Next articleMlinda Mlango wa Azam Anyakua Tuzo ya Mchezaji Bora Mlinda mlango wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Mwadini Ally amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo mwezi Machi baada ya kupata kura nyingi zaidi alizopigiwa na mashabiki wa timu hiyo. Mwadini ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwa na kiwango kizuri mwezi huo akicheza jumla ya mechi nne sawa na dakika 360 huku akiruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu. Kipa huyo amevuna asilimia 52 za kura 1,000 zilizopigwa na mashabiki wa soka kupitia ukurasa maalum wa kijamii wa Azam FC, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amevuna asilimia 25 huku Frank Domayo ‘Chumvi’ naye akivuna asilimia 23 ya kura hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here